• Karibuni Kenya
  • Flamingo wa waridi
  • Mapambazuko Savana
  • Pwani
  • Karibuni Kenya
  • Kuhubiri ufukweni mwa bahari
  • Karibuni Kenya
  • Karibuni Kenya
  • Jiji la Nairobi
  • Simba mwenye fahari
Iliyotangulia Ifuatayo

Jambo

Tungependa kuwakaribisha kwa uchangamfu kwenye Kusanyiko la Pekee la Mashahidi wa Yehova la Mwaka wa 2016, Nairobi, Kenya. Kusanyiko hili la pekee sana litatupa fursa ya kufurahia kitia moyo kizuri cha kiroho na ushirika wenye kujenga pamoja na wajumbe kutoka nchi mbalimbali. Tafadhali mnakaribishwa ili mfurahie uchangamfu wa ndugu na dada zetu wapendwa na pia hali nzuri ya hewa na mandhari maridadi ya Kenya. Tumeambatanisha picha chache zinazoonyesha baadhi ya mambo yenye kuvutia mtakayoweza kufurahia mkiwa wajumbe.

Tunathamini sana kuwa pamoja katika tengenezo la Yehova, kwa kweli ni paradiso ya kiroho. Tunatazamia kwa hamu kuunganishwa pamoja na kushangilia pamoja tunapolishwa kwenye meza ya kiroho ya Yehova. Karamu hiyo ya kiroho yenye kuburudisha katika Kusanyiko la Pekee la Mwaka wa 2016, itafanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Safaricom Kasarani, Nairobi. Tunaishi nyakati zenye kusisimua tukiwa undugu wa ulimwenguni pote. (Flp. 2:1, 2; 4:4)

Karibuni Sana Kenya!

Ndugu na dada zenu wapendwa nchini Kenya

Nembo

Tarehe

Desemba 2016

Nchi zilizokaribishwa

Ethiopia

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Marekani

Tanzania

Uganda

Ethiopia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Uganda Nairobi, Kenya Tanzania Marekani